Na Anthony  John Glob Ya Jamii. 

Watendaji katika Manispaa ya Kinondoni wakiwemo venyeviti wa mitaa wametakiwa kuwatumikia wananchi bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za vyama vyao.

Akitoa wito huo, mkuu wa wilaya hiyo ALI HAPI wakati akizungumza na watendaji wa kata ya Ndugumbi, amesema baadhi ya watendaji hasa wenyeviti wa mitaa katika baadhi ya sehemu wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwanabagua wananchi kwa itikadi za vyama vyao ,hali inayochangia pia kukosa huduma muhimu za kijamii.

Ametolea mfano upo mtaa mmoja ukionekana chama fulani hupati maji ,kwasababu kiongozi wa mtaa huo anatoka chama fulani na chama kingine huruhusiwi kuchota maji.

Ameeleza kuwa uchaguzi umekwisha, hivyo siasa na vyama vya siasa visiwagawe kwani hivyo husaidia ktk kuzipata nafasi hizo za uongozi tu.

Mkuu wa wilaya pia amekagua mradi wa ujenzi wa matundu 12 ya vyoo katika shule ya msingi Mwalimu Nyerere huku akimuagiza injinia wa manispaa hiyo SIMON LIACHEMA kuangalia mfumo wa kisasa katika utengenezaji wa matundu hayo ya vyoo ili kuwapa urahisi wanafunzi pindi wanapotumia vyoo hivyo.

Katika hatua nyingine amekagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu mkuu katika shule ya sekondari Turiani na kuahidi kutoa kiasi cha shilingi laki tano kwa walimu wa shule hiyo pindi watakapoanzisha chama chao cha kuweka na kukopa SACCOS pamoja na kutembelea soko la Babati.    


 .mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi  Akizungumza na wananchi katika soko Babati lililopo kinondoni Jijini dar es salaam.
 .Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi akikagua mradi wa majengo  mbali mbali katika  shule ya msingi Mwalimu Nyerere akiwa na walimu  wa Shule Hiyo leo hii iliyopo kinondoni Jijini Dar es salaam. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...