THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | CRDB BANK - THE BANK THAT LISTENS | NATIONAL BANK OF COMMERCE (NBC)- CONVENIENTLY EVERYWHERE | NATIONAL SOCIAL SECURITY FUND (NSSF) | PUBLIC SERVISE PENSIONS FUND (PSPF). ' Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Nawasihi kila mmoja wetu ajiheshimu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya GLOBU YA JAMII, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoelezwa vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.

Gadget

This content isn't available over encrypted connections yet.

'NILIAHIDI, NIMETIMIZA, NITAENDELEA KUTIMIZA' - RAIS JOHN POMBE MAGUFULI


MALKIA WA SHINDANO LA UREMBO KWA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI ‘ALBINO’ KENYA APATIKANA


Akina dada walioshiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.
Mamia walijitokeza kushuhudia maonyesho ya urembo ya Mr na Ms Albino nchini Kenya. Kila siku Albino wanakabiliwa na hatari ya kuuawa na viungo vyao vya mwili kuuzwa kutokana na imani za kishirikina Afrika mashariki na Afrika kusini.Chanzo-BBC SWAHILI
Malkia mpya! Louise Lihanda, aliyeshinda taji la urembo kwa akina dada atembea jukwani akiwa amevalia vazi la kupendeza lililotengenezwa kwa kutumia puto. Loiuse ambaye ni mwanafunzi, amekuwa mwanamke wa kwanza kushinda taji hilo, katika mashindano yaliyofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 21 Oktoba 2016
Wanaume walioshiriki katika mashindano hayo wasimama  jukwaani. walishiriki katika mashindano ya urembo kwa watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi ama Albinos jijini Nairobi, Kenya. Tarehe 21 Oktoba 2016.

Kutoka kulia, naibu rais wa Kenya William Ruto, Mbunge Isaack Mwaura na mkurugenzi mkuu wa bodi ya filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua pia walikuwemo.


MANGULA AFURAHISHWA 100 KUFUKUZWA UANACHAMA WA CCM MWANZA

Mzee Philip Mangula
Na Bashir Nkoromo, Mkuranga
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula ameelezea kufurahishwa kwake kufukuzwa kwa wanachama 100 mkoani Mwanza kwa kubainika kukisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

"Haiwezekani, unajiita mwanachama, halafu badala ya kujitolea kwa nguvu zako zote chama kishinde vita ya kushika dola, wewe unakisaliti,  hapo unakuwa si mwanachama bali jeshi la kukodiwa",  Mangula alisema, hayo jana, wakati akizungumza na Vijana wanaosoma na waliohitimu vyuo vikuu 20, ambao wameweka kambi ya kufyatua matofali kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari Nasabagani, Mkuranga mkoa wa Pwani.

 "Taarifa ya Chama kuwafukuza uanachama wale 100 kule Mwanza imenifurahisha sana, ni matumaini yangu kwamba hatua kama hizi zitaendelea kuchukuliwa  kila mahala nchini kote kwa waliokisaliti chama. hivi ni mchezaji gani anayempiga ngwara mchezaji wa timu yake wakati wa mechi ya kutafuta ubingwa halafu akaachwa kuendelea kuwa katika timu?" Mangula alisema na kuhoji kwa mshangao.

Mangua alisema, wakati mikoa itaendelea kuchukua hatua, lakini pia kwa ngazi ya taifa hatua dhidi ya waliokisaliti chama zitaendelea kuchukuliwa, ikiwa ni pamoja na kuwatupilia mbali watakaojaribu kuomba nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi wa Chama mwakani, huku wakiwa wameshabainika kuwa walikisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu ulipita.

Mangula aliwataka vijana nchini kote hasa wasomi, kuepuka kutumiwa vibaya na wanachama watakaokuwa wanasaka uongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa CCM unaotarajiwa kufanyika mwakani, kwa kuwa kijana yeyote atakayekubali kutumiwa vibaya atakuwa amekisaliti na kuchangia kunyong'onyesha nguvu na uhai wa Chama.

"Hili la kutumiwa vibaya hasa ninyi vijana, nawaasa sana kuepuka nalo, jambo hili ni baya sana, na si kwa Chama tu lakini hata kwa wewe uliyekubali kutumika, maana utatumiwa kama ngazi, halafu akishapita hatakuwa na manufaa kwako na hata kwa taifa maana atakuwa mvurugaji tu, badala ya kushiriki kuleta maendeleo ya chama na taifa", Alisisitiza mangula.


BALOZI WA AUSTRALIA NCHINI ATEMBELEA KIJIJI CHA DONGOBESH,MANYARABalozi wa Austraia nchini John Feakes akizungumza alipotembelea kijiji cha Dongobesh Mkoani Manyara, katika mradi wa FREO2 wa kuanzisha kituo cha kufua hewa ya oxygen kwa ajili ya kituo cha afya Dongobesh, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Chelestino Mofuga.


DC WA KILWA,MH.NGUBIAGAI AWAPA SIKU 14 WAVUVI HARAMU WAJISALIMISHE.

Mkuu wa wilaya ya Kilwa, Chistopher Ngubiagai, ametoa siku 14 kwa wavuvi haramu katika wilaya hiyo wajisalimishe na kukabidhi dhana wanazotumia.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo hilo wakati wa zoezi la uchomaji wa zana za uvuvi haramu lililofanyika mjini Kilwa Masoko.

Ngubiagai alisema uvuvi haramu nitatizo linalohitaji nguvu na jitihada zinazotokana na uzalendo ili kulikabili. Kwasababu ya mbinu zinazotumiwa na wahalifu katika kuhakikisha hawakamatwi na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Alisema mapambano hayo ni makali na magumu, kwa sababu baadhi ya wahalifu hao kuwa na mtandao mkubwa unaowahusisha baadhi ya viongozi na watendaji wa umma wasiowaadilifu. Hivyo wilaya hiyo imetengeneza mikakati madhubuti itakayotokomeza tatizo hilo linalotishia uwepo wa viumbe hai wa baharini. 

Ngubiagai aliitaja baadhi ya mikakati hiyo kuwa ni kuhakiki wavuvi wote waliopo katika wilaya hiyo na maeneo wanayofanyia shugulizao, kusajili vyombo vyote vya uvuvi na kuvipa namba za utambuzi na kujua kila chombo mahali kilipo, kuwasajili wavuvi wote walio kwenye kambi za uvuvi na kuainisha bandari maalumu zinazoshushia mazao ya uvuvi ya maeneo mbalimbali.

"Napenda kuwatahadharisha wasalimishe zana zao za uvuvi haramu haraka iwezekanavyo ndani ya wiki mbili kwani zama zao zimekwisha. Vita hii niliyoianza haitasimama nitahakikisha uvuvi haramu unatokomea kabisa katika wilaya hii,lengo ni kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinavinufaisha hata vizazi vijavyo," alisisitiza Ngubiagai.

Alibainisha kuwa kupitia hatua za awali za mapambano hayo ambayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Magufuli aliyotoa hivi karibuni jijini Mwanza, naya waziri mkuu, Kassim Majaliwa aliyotoa wilayani Mafia mkoa wa Pwani.

Wamefanikiwa kukamata kilo 281 za unga wa kutengenezea mabomu tambi 7, vibati 7 na chupa za mabomu ambazo zilikamatwa kutokana na ushiriano mkubwa wa raia wema kwenye kambi za uvuvi za Nyuni, Ukuza na Simaya.
"Unga uliokamatwa ulikuwa na uwezo wa kutengeneza chupa za mabomu 188,kila chupa ingeweza kuharibu eneo lenye ukubwa wa zaidi ya mita hamsini,maana yake nikwamba zisingekamatwa basi eneo la bahari lenye ukubwa wa zaidi ya mita za mraba 9400 zingeharibiwa kabisa," alisema.

Mkuu huyo wawilaya alitoa wito kwa serikali kupitia wizara ya maliasili na utalii kwa kusema "Kuna umuhimu wakuangalia na kutafuta uwezekano wa kuunda kikosi maalum cha kwa ajili ya kupambana na wavuvi haramu katika bahari na maziwa,kwa sababu hawa askari ingawa wanajitihidi sana na juhudi zao zinazaa matunda,lakini hawana uelewa mkubwa wa mambo ya bahari na sheria zake," alisema.

Kwa upande wake ofisa uvuvi wa halmashauri ya wilaya hiyo, Ahmad Mkali. Alisema miongoni mwa changamoto kubwa zinazosababisha kupunguza kasi ya kupambana na uvuvi huo ni uchache wa boti za kufanyia  doria.Akibainisha kuwa halmashauri hiyo inaboti moja tu. Wakati mahitaji halisi ni angalau boti nne."Wavuvi haramu wanavua bahari kuu ni mbali,na eneo la bahari nikubwa sana kwa boti moja inakuwa vigumu kuyafikia maeneo yote kwa wakati mmoja," alisema Mkali.
Baadhi ya zana haramu za uvuvi zilizokamatwa, Pichani ni Mabomu yanayotumika kulipulia Samakina viumbe vingine Baharini.

Zana Haramu za vuvi zikiteketea kwa moto. (Picha na :Bernad Mpangala Mchambuzi wa Mifumo Kilwa.)
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Ndg; Christopher Ngubiagai akizungumza na wavuvi.


MPAMBANO WA MISS TALENT 2016 JINSI ULIVYOFANA, MSHIRIKI LISA MDOLO KUTOKA SINGIDA AIBUKA KINARA

Miss Talent 2016 ambaye ni Mshiriki wa Miss Tanzania 2016 namba 20,Lisa Mdolo kutoka Singida (Kanda ya Kati) alishika nafasi ya Kwanza katika mpambano wa Kusaka Vipaji kwa washiriki wa Miss Tanzania 2016 uliofanyika Jembe Beach jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo. Mshindi huyo wa Miss Talent 2016 amecheza ngoma ya asili.
Top 5 Miss Talent 2016 wakiwa wamepozi mara baada ya kushinda nafasi tano Bora ya Miss Talent 2016.


Mamiss Tanzania 2016 wakionesha Vipaji vyao wakicheza  katika hafla ya Kutafuta Miss Talent 2016 leo jijini Mwanza.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii Mwanza.
WAZIRI MAKAMBA AKATAZA UCHEPUSHAJI WA VYANZA VYA MAJI


Na Lulu Mussa-Songwe

Wakazi wa Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wamehamasishwa kutunza Vyanzo vya Maji kwakuwa Maji hayana mmadala wa kitu chochote. Waziri wa Nchi mwenye dhamana ya Usimamizi wa Masuala ya Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba ameyasema hayo leo katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua mazingira nchini.

Akiwa katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje, Waziri Makamba alishuhudia uliochepushwaji wa Mto Kalembo kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, na haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Aidha Waziri Makamba amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kuhakisha wanambaini mtu/watu hao na kuwafisha katika vyombo vya Sheria.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa wilaya ya Ileje ilisema kwamba kumekuwa na uvamizi katika Vyanzo vya Maji na Serikikali imeendelea na juhudi za kuwaondoa kwa kuwapatia maeneo mengine ila baadhi ya wananchi hao wamekuwa wakikaidi. Hali hiyo haikumfurahisha Waziri Makamba na kuagizia kutumika mamlaka ya Dola. “Hatuwezi kuruhusu watu kuharibu Vyanzo vya Maji na kuwabembeleza watoke” Makamba alilisitiza.

Waziri Makamba amesema ni muhimu watu kutii Sheria na Mamlaka zilizopo, ameagiza wakazi hao kupewa wiki mbili tu na baada ya hapo waondolewe kwa nguvu kwani tayari maeneo mbadala kwa makazi yao yalisha ainishwa. Pia Waziri Makamba ameahidi kutoa muongozo wa Sheria ndogondogo za Mazingira za Vijiji na Vitongoji ili zitumike kama nyenzo za hifadhi ya Mazingira Nchini.

Katika hatua nyingine Waziri Makamba alitembelea Kijiji cha Lubanda, Kata ya Lubanda na kufanya Mkutano wa hadhara na wananchi na kuwasisitizia, kutokokata miti ovyo, kutochoma misitu na kuepuka uchepushaji wa Vyanzo vya Maji ikiwemo mito na Mabonde.

Pia Waziri Makamba aliwashauri wakazi wa Lubanda kulima kilimo cha Matuta ama makinga maji ili kuepuka mmomonyoko wa udongo katika miinuko. Aidha Waziri Makamba ameunga mkono jitahada za wananchi wa Kata hiyo za ujenzi wa Kituo cha afya kwa kuchangia bati Ishirini na nane (28). Waziri Makamba anaendelea na ziara yake na leo amewasili katika Mkoa wa Rukwa.

Uharibifu wa Mazingira unaofanywa na binadamu, pichani ni Mto Kalembo uliopo katika Kijiji cha Ibungu Wilayani Ileje uliochepushwa kwa manufaa ya baadhi ya mtu/watu, haikuweza kufahamika mara moja muhusika. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Ileje Bw. Joseph Modest Mkude kutafuta wahusika na kuwafikishwa kwenye Vyombo vya dola.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akifafanua jambo kwa wananchi mara baada ya kuwapa fursa ya kuuliza maswali katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Lubada Wilayani Ileje. Kushoto ni Bw. Stanford Kibona aliyeuliza swali.


VICHWA VYA HABARI YA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OKTOBA 23,2016


KICK BOXING BOUT IN NAIROBI: Emmanuel Shija [Tanzania] Vs Golola Moses [Uganda]


SHAMBA LA MITI LUNGUZA WAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI MUHEZA WAKABIDHI MADAWATI 200.


 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akikagua madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akitazama baadhi ya madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Meneja wa Shamba la Miti Lunguza,Abdallah Mchomvu akizungumza katika halfa hiyo ya kukabidhi madawati kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kushoto aliyekaa ambayo yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)
 Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza ambaye ni Afisa Tarafa ya Muheza Khatibu Omari wakati wa halfa hiyo wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Lunguza ambalo ni la serikali linalojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na ustawishaji wa miti ya misaji (Teak)
Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya MuhezaHajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo. 
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.


LATEST UPDATES FROM KC GLOBAL LINKS LTD


ILI KUBORESHA HUDUMA, SASA TUTAKUA TUNATUMA MZIGO KWA NDEGE MARA MBILI KWA WIKI.
AIR CARGO NO 1005 SASA KUONDOKA JUMATANO IJAYO IKIFUATIWA NA AIR CARGO 1006  JUMAMOSI IJAYO. 
KONTENA LA SEA CARGO NDIO LINAPAKIA SASA NA LITAONDOKA IJUMAA IJAYO. 
LETE MZIGO WAKO SASA.
AIR CARGO £3.50 inclusive clearance, 
Sea cargo £1.80 inclusive clearance
Tunafuata mzigo popote
Contact us:
KC GLOBAL LINKS LTD
SUITE 2 CLIPPER HOUSE
TILBURY PORT
TILBURY
RM18 7GS
Tel 01375 85 85 25
Mob: 07494364194


RC Arusha apokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Mashaka Gambo amepokea mifuko 500 ya simenti na mabati 500 kutoka kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kutoka Korea inayojenga barabara ya Tengeru - Sakina.

Msaada huo umetolewa ofisini kwake ambapo tukio hilo limeweza kushuhudiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa,Wilaya na Wabunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Arusha.

Akipokea msaada huo, Mrisho Gambo amesema atagawa mifuko 100 ya simenti na mabati 100 kwaajili ya ujenzi wa Zahanati kata ya Murieti kwasababu kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wagonjwa katika hospitali ya Mkoa Mt.Meru wanaotoka maeneo hayo hivyo ujenzi huo utasaidia  kupunguza wagonjwa katika hospitali hiyo.

Pia yatakayo baki atayapeleka Wilaya ya Longido katika kusaidia ujenzi wa bweni la shule ya sekondari Longido ambayo liliungua moto nakuteketeza kila kitu.

“Napenda kuishukuru na kuipotengeza kampuni ya ukandarasi ya barabara ya Tengure Sakina na ile ya njia mbadala(by path) kwakutoa msaada huu na kwakuwa tumeshaanza  mkakati wa ujenzi wa madara kwa shule za msingi na Sekondari,hivyo nitagawa hayo mifuko ya simenti 100 na mabati 100 ikajenge Zahanati kata ya Murieti na yaliyobaki yataenda Longido katika ujenzi wa bweni lililoungua”.

Mkurugenzi  Mtendaji wa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu bwana Xie Jianbao amesema kampuni yao imetoa msaada huo ikiwa ni moja ya shughuli zao zakusaidia jamii katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

“Tumetoa mifuko ya simenti 500 na mabati 500 kama moja ya mchango wetu katika kusaidia jamii yetu kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo”.

Aidha Mkurungezi wa Jiji la Arusha,Athumani Kihamia alisema  kutokana na wingi wa wananchi waliopo katika kata ya Murieti Zahanati hiyo itaenda kuwasaidia sana na kwakipindi kisichozidi miezi 2 Zahanati hiyo itakamilika na wananchi wataweza kuitumia.

Ukosefu wa kituo cha afya katika kata ya Muriet ulibainika baada ya Mkuu wa Mkoa Gambo kufanya ziara katika kata hiyo nakupata malalamiko kutoka kwa wananchi kuwa wanatembe umbali mrefu sana kutafuata huduma za afya.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akitoa shukrani kwa kampuni ya ukandarasi ya Hanil JV Jiangsu kwa kutoa msaada wa mifuko ya simenti 500 na mabati ya 500 kwa shughuli za maendeleo za Mkoa wa Arusha.
Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA


Wazalendo 53: Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara mzee Philip Mangula atembelea kambi la wazalendo wasomi

Makamu mwenyekiti wa ccm Tanzania Bara Mzee Philip Mangula akitembelea kambi ya Vijana 53 wazalendo Wasomi wetu kutoka vyuo vikuu vya nje na ndani ya nchi walioungana kwa pamoja kufyatua matofali 45,000 kwa ajili kujenga mabweni 5 pamoja na nyumba 5 za walimu katika shule ya sekondari Nasibugani wilayani Mkuranga, mkoani Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mh Filberto Sanga alichukua hatua ya kuandaa kambi hii ya wazalendo kusaidia adha waliyokuwa wakipata wanafunzi wa shule ya Nasibugani gani ikiwemo kukosa mahala pa malazi huku baadhi yao kidato cha tano na sita wakilala katika chumba cha maabara.
Ripoti iliyosomwa na Katibu Mkuu wa Wazalendo Bw Daniel Sarungi inaelezea maisha ndani ya kambi na shughuli walizofanya ikiwemo
 Kufyatua matofali, Kusomba Mchanga, Kujipikia chakula, Kufundisha wanafunzi wa kidato cha V na VI, Kutoa huduma ya afya kwa wanakambi na wanafunzi, Mijadala ya maendeo na utawala bora pamoja na Kuhamasisha wanafunzi kujiunga na vilabu vya kupinga rushwa.
Report hiyo ya wazalendo pia imeomba serikali kama ikiona inafaa wale wote wanaopenda kufanya kazi serikalini waanze kwa kujitolea miezi 6 au mwaka mmoja ndipo waajiriwe kufuatana na taaluma zao.
Kambi inaongozwa na mwenyekiti wa kambi Mwita Nyarukururu, Makamu Mwenyekiti ambae ni Helen Madole pamoja na Katibu Mkuu wa wazalendo Daniel Sarungi.
Mlezi wa kambi ya wazalendo ni kamati ya ulinzi na usalama wilaya ikiongozwa na Mh DC Filberto Sanga.

Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula katika picha ya pamoja na kambi la wazalendo wasomi
Kambi ya wazalendo ilianza tarehe 28/09/2016 na mpaka sasa zaidi ya matofali 38,235 yako tayari na yamebaki matofali 6,765 tu.
 Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula akichakarika na Wazalendo wasomi
 Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula akiendelea kufanya kazi  na Wazalendo wasomi
Makamu mwenyekiti ccm Tanzania Bara  mzee Philip Mangula akiongea na Wazalendo wasomi.


MKUTANO WA KWANZA WA BIASHARA NA UWEKEZAJI BAINA YA TANZANIA NA MOROCCO WAFANYIKA JIJINI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia kwenye mkutano wa Kwanza wa Wafanyabiashara wa Tanzania na Morocco utakaoainisha fursa za uwekezaji baina ya nchi hizo mbili uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.

Katika Hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa wafanyabiashara na Wawekezaji wa Tanzania na Morocco Makamu wa Rais aliainisha maeneo mbali mbali ambayo yanaweza kuwa fursa nzuri ya kuwekeza Tanzania.Baadhi ya maeneo hayo ni Kilimo,Utalii, Nishati, Mafuta na Gesi, Viwanda,Sekta ya Huduma, na Sekta ya Madini.Mbali na kuainisha baadhi ya fursa Makamu wa Rais aliwahakikishia uwepo wa amani na usalama na sheria mbalimbali zinazolinda haki za wawekezaji. 
Rais wa Chama cha Wafanyabiashara wa Morocco Bi.Miriem Bensalah-Chaqroun, akihutubia kwenye mkutano wa kwanza wa Biashara na Uwekezaji baina ya Tanzania na Morocco uliofanyika kwenye Hotel ya Hyatt Regency.
Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akizungumza wakati wa mkutano wa kwanza uliowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Morroco.
Sehemu ya wafanyabiashara kutoka Morocco wakifuatilia kwa makini mkutano huo.Rais Magufuli amteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi TAA  Prof. Ninatubu Mbora Lema

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Prof. Ninatubu Mbora Lema kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA).

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 22 Oktoba, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huu umeanza tarehe 20 Oktoba, 2016.

Prof. Ninatubu Mbora Lema anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Lambert Ndiwaita aliyefariki dunia tarehe 20 Agosti, 2015.

Prof. Ninatubu Mbora Lema ni Profesa Mshiriki Usimamizi wa Ujenzi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Associate Professor of Construction Management - University of Dar es Salaam).


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


22 Oktoba, 2016


YANGA WAIADHIBU KAGERA SUGAR BAO 6-2 KWENYE UWANJA WA KAITABA MJINI BUKOBA LEO

Yanga leo wameichakaza Kagera Sugar kwa idadi ya mabao 6-2 kwenye Mechi ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara, iliyochezwa katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba na kuchupa hadi Nafasi ya Pili.

Kagera Sugar ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 3 Mfungaji akiwa Mbaraka Yusuf na Yanga kusawazisha Dakika ya 4 kupitia Straika wao kutoka Zimbabwe Donald Ngoma.

Yanga walipa Bao la Pili Dakika 21 kupitia Simon Msuva na Straika wa Zambia, Obrey Chirwa, kuipa Bao la 3 Dakika ya 26.
Yanga waliongoza kwa Bao hizo 3 hadi Mapumziko.
Kipindi cha Pili, Dakika ya 49, Mbaraka Yusuf, kwa mara ya pili, akaipa Kagera Sugar Bao lao la Pili lakini Yanga wakaja juu na kupiga Bao 3 nyingine katika Dakika za 58, 63 na 64 kupitia Deus Kaseke, Chirwa na Ngoma.

Timu ya Pili ni Yanga yenye Pointi 21 kwa Mechi 10 wakifungana na Stand United, waliocheza Mechi 12, lakini wana udhaifu wa Magoli na hivyo kushika Nafasi ya 3.

Jumapili Oktoba 23 zipo Mechi 2 wakati Simba watakapocheza na Toto Africans ya Mwanza Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na huko Sokoine, Mbeya ni kati ya Tanzania Prisons na Mbao FC.
Mchezo huo umezalisha mabao nane ambapo Casillas alifungwa mabao matatu mepesi katika dakika 27 pekee alizokuwa langoni kabla ya Kocha Mecky Mexime kumtoa na kumuingiza David Burhan ambaye nae alifungwa matatu.

Cassilas alishindwa kujiamini langoni ambapo alifanya makosa kadhaa katika dakika chache alizodumu uwanjani ambapo kama washambuliaji wa Yanga wangeongeza umakini kabla ya mlinda mlango huyo kufanyiwa mabadiliko basi wangeweza kufunga zaidi ya mabao hayo kipindi cha kwanza.
Washambuliaji Obrey Chirwa na Donald Ngoma walifunga mabao mawili kila mmoja huku Simon Msuva na Deus Kaseke wakifunga moja moja na kukamilisha karamu hiyo ya mabao.


MANGULA ASHIRIKI KUFYATUA MATOFALI KUUNGA MKONO VIJANA WANAOSOMA NA WALIOHITIMU VYUO VIKUU 20

Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Mabweni ni kwa ajili ya Wanafunzi wa Kidato cha tano na cha sita, ambao kwa sasa wanalala chini katika chumba cha maabara ya shule hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula akisaidiana kubeba tofali na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga, baada ya kufyatua tofali hilo, wakati akishiriki kufyatua matofali leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani humo mkoa wa Pwani.
Mkuu wa wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani, Filbarto Sanga akimweleza jambo, Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula aliyetembelea eneo la ufyatuaji matofali kabla ya kushiriki ufyatuaji huo leo, kuunga mkono vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani. Kulia ni Mwenyekiti wa Kambi ya Vijana hao, Mwita Myamkururu.
Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula, akikagua matofali yaliyokwishafyatuliwa na vijana 53 wanaosoma na waliohitimu Vyuo Vikuu 20, walioweka kambi ya kufyatua matofali 45,000 kwa ajli ya ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu, katika shule ya Sekondari ya Nasabagani, iliyopo Kisiju, Wilayani Mkuranga mkoa wa Pwani Mkuu wa wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani, alipofika kuwaunga mkono vijana hao leo. Nyuma yake ni Mkuuwa wilaya ya Mkuranga, Filbarto Sanga na katibu Msaidizi wa CCM mkoa wa Pwani, Abiudi Shilla. Picha zote na Bashir Nkoromo-Official CCM Blog. PICHA ZINGINE KEM KEM ZA TUKIO HILI/>>BOFYA HAPA


Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli ya Kitalii katika Kijiji cha Matemwe Zanzibar Inayojengwa na Pennyroyal (Gibraltar) Ltd Zanzibar.

 
 
Mmiliki wa Mradi wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mkurugenzi wa Mradi huo Brain Thomson, akitowa maelezo kwa waandishi wa habari walipofika kutembelea mradi huo kujionea maendeleo ya matayarisho yake na kuwaonesha michoro ya picha za majengo ya Mradi huo mkubwa utakaokuwa na uwanja vya ndege. na kutengeneza visiwa kwa ajili ya wageni wanaofika katika Visiwa vya Zanzibar. 
Mmiliki wa Mradi wa Mkubwa wa Hoteli ya Kitalii katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson, akitowa maelezo ya mradi huo kwa kuwaonesha jinsi ya majengo yatakuwa katika eneo hilo na kutoa ajira kwa Wananchi wa Matemwe na vijiji jirani kupitia mradi huo. 
Mmiliki wa Mradi Mkubwa wa Ujenzi wa Hoteli katika eneo la Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja Mr. Brian Thomson akizungumza na waandishi wa habari walipofika kuangalia ujenzi wa mradi huo na kusema kukamilika kwakev kutachukua miaka minane kukamilika kwake na kutowa fursa za ajira kwa vijana wa kijiji hicho na kutowa maendeleo katika sekta za jamii kunufaika na mradi huo.

PICHA ZAIDI BOFYA HAPA