Mkuu
wa Mwanza, John Mongella akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko
wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, wakati alipofanya ziara yake ya
kwanza ya kutembelea ofisi za taasisi mbalimbali za umma jijini humo.
Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe akitoa
maelezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, namna Mfuko huo
unavyofanya kazi, ambapo alisema kuwa mfuko huo sasa unawalipa mafao
wanachama wake kwa wakati ambapo umevuka
lengo kwa kukusanya michango ya shilingi bilioni 17.03 kati ya shilingi
bilioni 17.6 za lengo kwa mwaka jana ulioishia juni 2016. Bandawe
alimweleza mkuu huyo wa mkoa kuwa mfuko wa PPF umefanikiwa kusajili
wanachama wapya 13,028 kwa Kanda ya Ziwa pekee ikiwa ni sawa na asilimia
105 ya lengo
la kusajili wanachama 12,350 kwa kipindi cha mpaka juni 2016.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akiangalia Kadi yake ya Uanachama wa
PPF aliyokabidhiwa na Meneja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa,
Meshach Bandawe.
Meneja
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe akimkabidhi
Kadi ya Uanachama wa PPF, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Ahmed
Msangi.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella akipatiwa maelezo na Meneja wa Mfuko
wa Pensheni wa PPF Kanda ya Ziwa, Meshach Bandawe (shati jeupe) wakati
alipotembelea moja ya Idara ya Mfuko huo, Jijini Mwanza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...