Sehemu ya magari tisa yaliyotolewa na shirika la EGPAF.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
CHUO cha Ufundi Cha VETA Chang'ombe kimepata msaada wa magari tisa kutoka katika shirika la Elizabeth Glasser Padiriatic Foundation (EGPAF) yatakayotumika kwa ajili kujifunzia wanafunzi katika chuo hicho.
CHUO cha Ufundi Cha VETA Chang'ombe kimepata msaada wa magari tisa kutoka katika shirika la Elizabeth Glasser Padiriatic Foundation (EGPAF) yatakayotumika kwa ajili kujifunzia wanafunzi katika chuo hicho.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam, Habib Bukko amesema kuwa msaada wa magari ni mkubwa kutokana na changamoto walikuwa wanakabiliana nayo.
Bukko amesema kuwa chuo cha ufundi kimekuwa hakina magari ya kutosha kwa ajili ya kujifunzia na taratibu za serikali zinataka magari yanunuliwe mapya lakini msaada huo ni hatua moja nzuri ya kusaidia chuo hicho.
Amesema kuwa watu wengine wenye mashirika wanaweza kuwasaidia magari yao ambayo wanataka kuyauza kwani kwao ni msaada mkubwa kutokana na mahitaji yaliyopo katika zaidi vyuo 700 vya ufundi.
Aidha ameesma kuwa zaidi vijana milioni 25 wanahitaji kupata mafunzo hivyo kuna umhimu wa kuwa rasilimali ya vifaa katika kuweza kuendana na idadi hiyo.
Nae Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EGPAF, Jacquesdol Massawe amesema kuwa wanatambua umhimu magari hayo kwa ajili ya kuwafundishia vijana wakitanzania na kuweza kupata ujunzi na kuja kutumika katika uzaslishaji.
Amesema uchumi wa viwanda unahitaji kuwa rasilimali watu wenye ujuzi kuweza kutumika katika uzalishaji wa viwanda hivyo.
Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam wa VETA, Habib Bukko akizungumza na
waandishi habari juu ya msaada wa magari tisa yalitolewa na Shirika la
EGPAF leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EGPAF, Jaccquesdol Massawe akizungumza juu
ya msaada magari tisa jinsi yatavyotumika katika kufundishia vijana
vyuo vya VETA, leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha VETA
Changombe, Douglas Kipokola akizungumza namna ya kuyatumia magari hayo
katika chuo hicho leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kanda
ya Dar es Salaam wa VETA, Habib Bukko akipokea nyaraka za magari hayo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji wa EGPAF, Jaccquesdol hatika hafla
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...