Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na
Mkewe Mama Janeth Magufuli wakimjulia hali Mzee Francis Maige Kanyasu(Ngosha)
aliyelazwa Wodi ya Mwaisela katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam kwa ajili ya
Matibabu leo. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili Profesa Lawrence Museru pamoja na Dkt. Juma Mfinanga Daktari Bingwa
wa magonjwa ya Dharura na Ajali katika hospitali hiyo.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth
Magufuli wakimjulia hali mtoto Shukuru Kisonga aliyelazwa katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili. Mtoto Shukuru alikuwa akidaiwa kuishi kwa kula Sukari,
Maziwa na mafuta ya kula lakini hali yake imeimarika zaidi na kuanza kula
vyakula vya kawaida. Katikakati ni Mama yake Shukuru Mwanahabibi Mohamed Mtei.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine
waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwajulia hali wagonjwa wengine waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA Angalia video hapo chini |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...