Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akimkabidhi mpira wa miguu mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo. Wa kwanza kusho to ni Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Msingi Wailes, Zabibu Wasia akishuhudia. Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah (kushoto) akitoa elimu ya masuala ya kifedha na akiba kwa wazazi na wanafunzi walioshiriki mafunzo ya programu ya wajibu ya NMB katika Shule ya Msingi Wailes ya jijini Dar es Salaam. Mmoja wa wachezaji vijana (kulia) wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Azam kupitia kituo chao cha michezo akimkabidhi mpira wa pete mmoja wa viongozi wa michezo wa Shule ya Msingi Wailes kwa ajili ya shule hiyo. Mpira huo umetolewa na Benki ya NMB kama zawadi kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes mara baada ya elimu ya masuala ya fedha na akiba iliyotolewa na benki hiyo.
Mmoja wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes akijibu swali kwenye mafunzo ya programu ya wajibu iliyotolewa na Benki ya NMB shuleni hapo.

BENKI ya NMB imetoa elimu ya masuala ya kibenki na umuhimu wa kujijengea utamaduni wa uwekaji akiba kwa wanafunzi na baadhi ya wazazi wa Shule ya Msingi Wailes iliyopo Temeke jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes walioshiriki mafunzo hayo ya kifedha, Ofisa wa Benki ya NMB Tawi la Temeke, Latifa Ayoub Dadah alisema NMB inaendelea kutoa elimu ya masuala ya kifedha ikiwa ni pamoja na kujifunza mbinu za kuweka akiba kwa ajili ya maisha ya baadae. 

Alisema elimu hiyo inatolewa kupitia Programu maalum ya Wajibu ambayo hutoa fursa kwa watoto, vijana na wazazi kujifunza masuala ya kifedha ili kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba, elimu ambayo watoto wengi hawapati fursa ya kujifunza. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...