Na Lydia Churi, Songea
Katika ziara hiyo Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mheshimiwa Ferdinand Wambali amesema Mahakama itashirikiana na wadau wake ili kuhakikisha kesi zinamalizika kwa haraka kwenye mahakama mbalimbali nchini. 
Amesema kupitia nguzo ya tatu ya Mpango Mkakati wa miaka mitano wa mahakama ya Tanzania ambayo inasisitiza kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama, Mahakama itatoa elimu kwa wananchi pamoja na viongozi wakiwemo wakuu wa wilaya juu ya masuala mbalimbali yanayohusu utoaji wa haki kwa wananchi. 
 Jaji Kiongozi amesema Mahakama imejiwekea mikakati ya kuhakikisha kesi zinamalizika kwa wakati na kwa haraka ukiwemo mkakati wa kesi kutokukaa kwa zaidi ya miaka 2 kwenye Mahakama Kuu, miezi 12 Mahakama za mikoa na Wilaya pamoja na miezi sita kwenye Mahakam za Mwanzo. Mikakati mingine ni ile ya kesi kusikilizwa kwa mfululizo na kuwekwa kwa maahirisho mafupi mafupi ya kesi kwenye Mahakama mbalimbali nchini na Majaji na Mahakimu kupangiwa idadi ya kesi watazosikiliza katika kipindi cha mwaka moja. 
Aidha, kila Jaji amepangiwa kusikiliza na kumaliza kesi 220 kwa mwaka ambapo Mahakimu wamepangiwa kumaliza kesi 250 kwa mwaka. 
Akizungumzia Maadili kwa watumishi wa Mahakama, Jaji Wambali amewataka watumishi hao kuwahudumia wananchi wanaofika mahakamani kwa bidii, uaminifu, na uadilifu ili kujenga imani ya wananchi kwa Mahakama. 

Amesema watumishi wa Mahakama hawana budi kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano kwa kuwa kazi za mahakama zinategemeana ambapo kila kada ina umuhimu wake katika wananchi kufikia haki zao za msingi.
 Jaji Kiongozi yuko kwenye ziara katika kanda za Songea na Mtwara kwa ajili ya kukagua shughuli za kimahakama pamoja na kusisistiza utekelezaji wa Mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania. Tayari ametembelea mahakama zilizoko Songea mjini na zile za wilaya za Mbinga, Nyasa, Namtumbo, na Tunduru.

 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Ruvuma (Hawapo Pichani) wakati alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge ofisini kwake akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea. 
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Binilith Mahenge akizungumza
 Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Ferdinand Wambali akizungumza na Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (Hawapo Pichani) akiwa katika ziara ya kukagua shughuli za Mahakama na Kusisitiza Utekelezaji wa Mpango Mkakatiwa Miaka Mitano wa Mahakama ya Tanzania katika Kanda ya Songea. 
Mtendaji wa Mahakama, Samson Mashalla akifafanua masuala mbalimbali yanayohusu Utumishi kwa Watumishi wa Mahakama Kuu kanda ya Songea (hawapo pichani) wakati wa ziara ya Jaji Kiongozi kwenye kanda hiyo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...