Sensei Rumadha Fundi, mwakilishi wa Jundokan So Honbu Tanzania, na wanafunzi waandamizi toka " Jamhuri Kaizen Dojo na Zanaki Dojo " za Dat es salaam wanakitarajiwa kupandishwa ngazi ya chama hicho baada ya semina ya
(European Jundokan Gasshuku) Mnamo mwezi July 14 hadi 16, 2017. katika mji wa Marki, nje kidogo ya mji wa Warsaw, Poland.
Hali kadhalika Sensei Rumadha amepewa mwaliko huo ikiwa ni sehemu ya kwenda kukutana na walimu wakuu ( Masters) toka Okinawa, Japan, na kufanya mtihani wa shahada ya nne "Yondan" ya Goju Ryu chini ya mwenyekiti wake, Master Kancho Yoshihiro Miyazato.
Maandalizi makubwa yanatarajiwa kwa wanafunzi wa Tanzania ambapo hatimaye watapandishwa ngazi za ualimu za " Sensei " mara baada ya Sensei Rumadha kuwasili nchini baada ya semina hiyo ya Poland.
Sensei Rumadha na wanafunzi wake wa wakilishi wa Tanzania Senpai Waheed na Senpai Jesse wakiwa mazoezi jijini Dar es salaam ni hivi karibuni.
Sensei Rumadha na wanafunzi wa Zanaki Dojo wakiwa mazoezi jijini Dar es salaam ni hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...