First National Bank (FNB) Tanzania imeendelea kupanua wigo wake kitaifa kwa kufungua tawi jipya eneo la PPF Plaza jijini Arusha kwa lengo la kuhudumia ongezeko la idadi ya wateja katika mkoa huo.

 Akizungumza wakati wa ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo, Dave Aitken alisema uzinduzi wa tawi la FNB Arusha umelenga kukidhi ongezeko kubwa la wateja na mahitaji ya huduma za kibenki na kifedha katika kanda ya kaskazini. 

“ Uzinduzi wa tawi la Arusha ni sehemu ya mkakati wa uwekezaji endelevu uliolenga kuhakikisha maeneo mengi ya nchi yanapata huduma bora za kifedha. Pia ni kwa maslahi ya ukuaji wa haraka wa mkoa wa Arusha ambao una mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa Tanzania” Aitken alisema tawi la Arusha ni la kumi miongoni mwa mtandao wa matawi ya FNB Tanzania ikiwa ni sehemu ya mpango mkakati wa kupanua mitandao ya matawi kwa kusudi la kuyafikia maeneo mengi ya nchini.

 “First National Bank (FNB), daima tunafikiria njia ambazo zinaweza kutoa huduma za kibenki kwa urahisi kwa wateja wetu. Tawi letu la Arusha litasaidia kuwapatia huduma zote za kibenki wananchi wa mkoa wa Arusha na wanaoishi maeneo jirani kwani maeneo haya yote yamedhiirika kuwa na biashara mbalimbali zinazokua kwa kasi,” alisema Aitken. 
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akikata utepe kuzindua rasmi tawi la benki ya FNB Tanzania la Arusha huku akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqqaro (wa kwanza kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa FNB, Dave Aitken(wa pili kushoto) na Meya wa Jiji la Arusha, Mh. Calist Bukhai (kulia). 
Meneja wa Tawi la FNB Arusha, Genevieve Massawe akimueleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dr. Ashatu Kijaji jinsi mashine ya kisasa ya kuweka fedha (cash deposit) na kutoa fedha. Mashine hiyo ya kisasa inamuwezesha mtumiaji kuweka fedha zake benki muda wa masaa 24 imewekwa kwenye tawi hilo jipya ili kuwawezesha wananchi kuweka akiba fedha zao muda wowote ule. 
Afisa Mtendaji Mkuu wa First National Bank, Dave Aitken akimrekebishia kipaza sati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati wa uzinduzi rasmi wa tawi la FNB Tanzania la Arusha mwishoni mwa wiki. 


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...