Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Idi amewaasa wana CCM na wananchi nwote Nchini kuacha tabia ya kuhamanika kutokana na uvumi unaoenezwa mitandaoni kwamba yapo mabadiliko ya utawala wa Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

Alisema Wananchi wanapaswa kuelewa kwamba uchaguzi Mkuu wa Zanzibar umekwisha kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya Mwaka 1984 na kuwataka kuelekeza nguvu zao katika kusimamia mirai yao ya maendeleo.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa nasaha hizo wakati akitoa salamu kwenye Hfla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu za Soka zitakazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo hapo ukumbi wa CCM Mkoa Amani Mjini Zanzibar ambapo Mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.

Aliwatanabahisha wale wote wanaoendeleza kasumba ndani ya mitandao ya Kijamii kwa kuwadanganya Wananchi kwa makusudi waendelee kuvumilia na kustahamili hadi utakapofika uchaguzi mwengine Mkuu wa Mwaka 2020.

Balozi Seif Ali Iddi ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwahakikishia Wazanzibari na Watanzania wote kwa jumla kwamba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ataendelea kuviongoza Visiwa vya Unguja na Pemba hadi utakapofanyika uchaguzi mwengine mwaka 2020 kama Katiba ya Zanzibar inavyoeleza.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif Ali Iddi akitoa salamu katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Michezo kwa Timu zinazoshiriki Mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja hapo ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Wanamichezo wa Timu za Majimbo wakifuatilia hafla ya ugawaji wa vifaa vya michezo kwa Timu zao hapo Ukumbi wa CCM Mkoa Aman Mjini Zanzibar.
Kikundi cha Utamaduni cha CCM Mkoa Mjini Big Star kikitoa burdani wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa timu zinazoshiriki mashindano ya Ligi ya Majimbo Unguja ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamuj Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein.
Balozi Seif akisalimiana na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mkoa Kusini Unguja Mh. Mohamed Raza ambae ia ni mdhamini wa mashindano ya Kombe la Jimbo Unguja nje ya ukumbi wa CCM Aman Mjini Zanzibar.Picha na – OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...