Na Tiganya Vincent, MAELEZO- Dar es salaam

Wasomi na Wanazuoni mbalimbali wamepongeza hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri Mkuu zamani Edward Lowassa kushikana mikono na kusalimiana wakati wa Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya ndoa ya Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na Anna Mkapa.

Wanazuoni hao wametoa kauli hiyo leo katika mahojiano maalum na Idara ya Habari iliyokuwa ikitaka kupata maoni yao kuhusu kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwa jamii.Profesa Kitila Mkumbo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa huo ndio Utanzania ulivyo wa kutofautiana bila kugombana.
Amesema kuwa kitendo hicho kimewaonyesha wananchi kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa ya kuondoa tofauti zilizopo kuliko kutumia njia nyingine kama vile maandamano na mabavu katika kutafuta ufumbuzi wa baadhi ya matatizo.“Kukutana kwa viongozi hao na kupeana mikono wakati wa kusalimiana kunakumbusha utamaduni wetu uliojingekea toka siku nyingi wa kutatua matatizo yetu kwa mazungumzo bila kugombana au kutumia mabavu,”alisema Profesa Mkumbo.
Kwa upande wa Profesa Joseph Semboja amesema kuwa amefurahishwa sana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao kwani kimeuonyesha ulimwengu kuwa Watanzania ni watu wenye Amani na upendo.Amesema kuwa hatua hiyo imeonyesha kuwa Watanzania wanaweza kuwa na tofauti lakini wakaendelea kuishi pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali ya kijamii kwa ajili ya maendeleo yao na Taifa lao.
Profesa Semboja amewataka wananchi kujifunza kutokana na kitendo kilichoonyeshwa na viongozi hao ambao wameonyesha kuwa ni lazima wakae pamoja kwa ajili kushughulikia mambo muhimu ya maendeleo ya wananchi badala kuendeleza tofauti ambazo hazina manufaa kwa Watanzania.
Amesema kuwa ipo haja ya kwenda zaidi ya hapo kwa kuweka utaratibu wa kukaa pamoja na kujadiliana ili kutatua vyanzo vya migogoro kwa ajili ya mustakabali mzuri wa Taifa hili.Profesa amesema kuwa sio sahihi kutumia mfumo wa jino kwa jino kwani utaratibu huo ndio unaoweza kusababisha kukua zaidi kwa migogoro na wakati mwingine unasababisha umaskini kwa wananchi na Taifa kwa ujumla kwani muda mwingi wananchi hawana muda wa kushiriki katika shughuli za maendeleo kwa sababu ya migogoro.
Naye Profesa Samwel Wangwe amesema kuwa hatua ya viongozi hao kukutana na kupeana mikonop ni ishara kwa Watanzania kujifunza kuwa mazungumzo yana nafasi kubwa katika kuleta muafaka mgogoro wowote kuliko kutunishiana misuli.
Amesema kuwa mazungumzo yana nguvu kubwa katika kultea upatanishi katika migogoro mbalimbali inatokea katika jamii kuliko kutumia njia nyingine ambazo zinaweza kusababisha vurugu na uharibifu wa mali za watu na upotevu wa maisha ya watu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. SHUJAA ANAYE JITAHIDI KUTATUWA MATATIZO YAKE, ANAFAIDIKA NA UWEZO WAKE. NAOMBA VIONGOZI MJUWE YA KUWA MKIFANYA WATU WAJUWE KWAMBA MNAANGALIA MAZURI YAO KABLA YA MABAYA YAO WATAKUBALI NASIHA ZETU.
    DR,JAMESY.

    ReplyDelete
  2. Mie hii imenifurahisha na kunipa matumaini makubwa..
    Nionavyo mimi ni kwamba hawa jamaa walioondoka kwenye chama ni kama ndugu wanapogombana kwa sababu fulani, na sababu hiyo ikisha pita, ndugu hukaa kitako na kuondoa ukorofi wao.Ukorofi kumbuka ulikuwa ni uchaguzi na sasa uchaguzi imesha pita. Chama kingeweza kuonyesha example of wisdom and tolerance na kuwakaribisha hawa jamaa wote wasahau ugomvi na kurudi nyumbani. We are waiting for the return of the PRODIGAL SON (Luke 15:11-32)
    ibrahim

    ReplyDelete
  3. Kama litatokea shindano la wenye mioyo ya uvumilivu basi Lowassa wenda akawa nafasi za juu zaidi.Kila mtu ametafsiri anavyojua yeye tukio hili......

    ReplyDelete
  4. Ni kweli inapendeza mnoo

    ReplyDelete
  5. All these are mere speculation kwakua hakuna anaeweza kithibitisha lolote zaidi ya salam na kupeana mikono ambao ni ustaarabu wa kawaida . watanzania tumekuwa watu wa kutengeneza maneno na kutaka jamii iamini hata yasiyokuwapo.
    Ninahakika si raisi au ndugu Lowasa ameshasema lolote kuhusiana na hili!

    ReplyDelete
  6. Naunga mkono maoni ya mdau wa 5. hapo juu. Kama alivyosema salam na kupeana mikono ni ustaarabu wa kawaida, pia ni mojawapo ya utamaduni wetu katu hilo hatuliepuki ukizingatia...salamu siku zote haigombi. Hapo hakuna ithibati yeyote inayoonyesha muafaka zaidi ya kusalimiana. Kukutana kwenye 'hafla' hiyo sio kuwa ndio kigezo au chambo cha utathmini chanya, nadhani kwa tukio hilo moja kwa moja wameweza kuonyesha mfano mzuri wa ukomavu na ustaarabu wao katika kiwango cha hali ya juu licha ya kuwepo kwa tofauti zao za kiitikadi in whatever aspect. Katika hafla hiyo Mh. Rais JPM alisema kufuatia tukio hilo, kama ni muujiza basi na hilo ni miongoni mwa muujiza huo uliyoweza kujitokeza siku hiyo. Kwa hiyo ni mapema mno kuanza kutabiri mwelekeo na khatma kukhusiana na hilo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...